Raisi Wa Marekani Aongeza Idadi Ya Wakimbizi Wanaoingia Marekani
Raisi Wa Marekani Aongeza Idadi Ya Wakimbizi Wanaoingia Marekani

Rais Joe Biden ametangaza, baada ya kukosolewa vikali, kuwa anaongeza idadi ya juu ya wakimbizi wanaoruhusiwa kuingia Marekani mwaka huu hadi 62,500 — kutoka idadi ya ukomo ya 15,000 iliyowekwa na mtangulizi wake Trump.


Mabadiliko hayo yanafuatia upinzani kutoka kwa washirika kuhusu uamuzi wa awali wa Biden wa kudumisha viwango vya enzi ya Trump.

Biden amesema katika taarifa kuwa hatua yake inafuta idadi ya chini ya kihistoria iliyowekwa na utawala wa awali ya 15,000, ambayo haikuonyesha maadili ya Marekani kama taifa linalowakiribisha na kuwasaidia wakimbizi.

Mpango huo unahusu tu wakimbizi wanaochaguliwa la mashirika ya Marekani ya usalama na intelijensia kutoka kambi za Umoja wa Mataifa kote duniani. Utawala wa Biden unakusudia kuongeza ukomo wa hadi idadi ya juu Zaidi ya wakimbizi 125,000 katika mwaka ujao wa kifedha.