Mwanamke Ajifungua Watoto Tisa
Mwanamke Ajifungua Watoto Tisa

Mwanamke mmoja nchini Mali amejifungua watoto tisa katika hali ambayo sio ya kawaida.

Halima Cisse, 25, alijifungua watoto wa kike watano na wavulana wanne katika hospitali ya Morocco siku ya Jumanne ambako alikuwa amelazwa, Waziri wa Mali Fanta Siby alisema katika taarifa. Alijifungua kupitia njia ya upasuaji.

Bi Cisse amekuwa akitarajia kijifungua watoto saba kulingana na uchunguzi wa skani ya tumbo aliyofanyiwa nchini Mali na Morocco lakini skani hiyo haikugundua amebeba watoto wengine wawili.

Siku ya Jumanne, Dkt Siby alisema watoto hao na mama yao “wanaendelea vyema”. Wanatarajiwa kurejea nyumbani wiki chache zijazo.

Aliwapongeza madaktari waliomhudumia Mali na Morocco, “ambao ujuzi wao ni chanzo cha matokeo mema ya ujauzito huu”.

Mimba ya Bi Cisse imeshangaza taifa hilo la Afrika Magharibi na imewavutia baadhi ya wakuu wa nchi hiyo – huku baadhi yao wakisafiri had Morocco alipohitaji utunzi wa kitaalamu, shirika la habari la Reuters liliripoti.

Msemaji wa wizara ya afya ya Morocco, Rachid Koudhari, ameliambia shirika la habari ya AFP kwamba hakujua uzazi wa aina hiyo hutokea nchini humo.