Kampuni Ya Ndege Tanzania, Atcl Yasitisha Safari Zake Kwenda India
Kampuni Ya Ndege Tanzania, Atcl Yasitisha Safari Zake Kwenda India

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imesitisha safari zake za ndege kati ya Dar es salaam na Mumbai (India) kuanzia May 04,2021 hadi itakapotolewa taarifa nyingine ya kurudisha safari hizo hii ni kutokana na kuwepo kwa ongezeko la maambukizi ya Corona nchini India

“Abiria wote wenye tiketi za ATCL katika safari za DSM- Mumbai wanashauriwa kuwasiliana na Ofisi za ATCL au Mawakala wao kwa taratibu za kubadilisha tiketi ili zitumike pindi safari zitakaporejea tena bila gharama yoyote, tunaomba radhi kwa usumbufu” ATCL