Hatuna Hofu Dhidi Ya Simba - Mabeki Wa Yanga
Hatuna Hofu Dhidi Ya Simba - Mabeki Wa Yanga

Mabeki wa kati wa kikosi cha Yanga wameweka wazi kwamba hawana hofu kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Mei 8, Uwanja wa Mkapa.
Ni Abdalah Shaibu, ‘Ninja’ chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nassredine Nabi na Dickson Job ambaye ni beki chipukizi ndani ya kikosi hicho kinachowania kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.
Ninja ambaye amekuwa kwenye ubora katika mechi za hivi karibuni amesema kuwa hana hofu kuelekea katika mchezo huo na anaamini kwamba watafanya vizuri.
“Hakuna haja ya kuwa na hofu kwa sababu tunawajua vema wapinzani wetu na kikubwa ni kujiamini na kufanyia kazi yale ambayo mwalimu ametuambia.
“Tumekutana nao katika mechi zetu za hivi karibuni na tunajua kwamba nao watakuwa wanahitaji pointi tatu kama ambavyo nasi tunazihitaji, mashabiki watupe sapoti,”.
Job amesema kuwa kwa mbinu ambazo wanapewa na Nabi wanaamini kwamba watafanya vizuri kwenye mchezo huo.
Kwenye msimamo Yanga imekusanya pointi 57 baada ya kucheza jumla ya mechi 27 inakutana na Simba yenye pointi 61 ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 25.